HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA IDARA YA MIFUGO
KITENGO CHA MIFUGO.
HUDUMA ZA UGANI
Kutoa elimu kwa wafugaji juu ya kanuni bora za ufugaji ili kuinua kiwango cha uzalishaji wa mazao mbalimbali ya mifugo (maziwa, nyama, mayai na ngozi)
UKAGUZI WA NYAMA.
Kuhakikisha afya ya jamii inalindwa kupitia ukaguzi wa nyama za mifugo yote inayochinjwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
AFYA YA MIFUGO
Mifugo yetu kama mojawapo ya viumbe hai, idara inahakikisha afya zao zinaangaliwa kupitia uzuiaji ueneaji wa magonjwa ya kuambukiza kwa kusimamia na kutoa chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mifugo, kuudhibiti wadudu waenezao magonjwa na kutoa tiba za magonjwa mbalimbali ya mifugo. Hii ni katika kuhakikisha mifugo inakuwa na afya nzuri ili kuinua kiwango cha uzalishaji.
HUDUMA ZA MIFUGO
Kutoa huduma mbalimbali za mifugo kama vile; kuhasi, kukata pembe, kukata mikia, kukata kwato,kukata midomo, kukata meno, kupima mimba, kuhamilisha, kuchoma sindano ya kuchochea joto na madini ya chuma; kumsaidia mfugo kuzaa na kutoa kondo la nyuma.
UPATIKANAJI WA MALISHO NA MAJI
Kusimamia utengaji wa maeneo ya kutosha kwa ajili ya malisho na maji.
Kutatua migogoro inayotokana na malisho.
UTAMBUZI, USAJILI NA UFUATILIAJI WA ALAMA ZA MIFUGO
Kutambua mifugo yote ilinayofugwa katika Wilaya, kuisajili na kuipiga chapa kwa lengo la kusimamia uhamishaji wa mifugo kutoka eneo moja kwenda eneo jingine, kudhibiti ueneaji wa magonjwa ya mifugo na kufuatilia mifugo inayopotea au kuibiwa.
UKUSANYAJI WA MADUHULI YA SERIKALI.
Ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kuu kupitia utoaji wa vibali vya kusafirisha mifugo na mazao yake.
Ukusanyaji wa maduhuli ya Halmashauri kupitia utoaji wa vibali vya biashara za mifugo na mazao yake.
KIBONDO DISTRICT COUNCIL, KIBONDO TOWNSHIP IHULILO STREET
Anuani ya Posta: P.O.BOX 43, KIBONDO
Simu ya Mezani: +255 028 282 0084
Simu: +255 028 282 0084
Barua pepe: ded@kibondodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Kibondodc .Haki zote zimehifadhiwa.