Mkuu wa Mkoa Kigoma Mhe. Brigedia: Emanuel Maganga, amefanya kikao na Wananchi wa Wilaya Kibondo, walioathiriwa na ujio wa Wakimbizi kwa awamu ya pili katika Wilaya ya Kibondo kwenye Ukumbi wa Vijana maarufu kama Jumba la Maendeleo leo tarehe 06.09.2018.
Kikao hicho kilihusisha Wananchi waliokuwa wakilima ndani ya kambi hiyo baada ya wakimbizi wa awamu ya kwanza kuondoka, pamoja na waliojikuta wamo ndani ya kambi hiyo baada ya upanuzi wa kambi. Hao ndio waliofanyiwa Tathimini ya mali zao zilizokuwemo katika maeneo hayo kwa jitihada za Serikali ili wapewe fidia.
Akizungumza na Wananchi hao Mkuu wa Mkoa Kigoma, alisema " Tulifanya jitihada kubwa ili kupata namna ya Wananchi wetu fidia ya mali zao zilizoathiriwa kutokana na Ujio wa Wakimbizi katika Wilaya ya Kibondo ndani ya Kambi ya Nduta, jitihada hizo nilifanya mimi kwa kushirikiana na Uongozi wa Wilaya ya Kibondo na Wizara husika, ili kupata mtu anayeweza kulipa gharama hizo zilizotokana na tathmini ya mali za wananchi hao. kwa bahati nzuri shirika la Kimataifa la wakimbizi la UNHCR lilikubali kulipa fidia hiyo kwa sharti hili; Watamlipa mhusika mwenyewe mwenye mali, moja kwa moja na hela haitapitia kwenye akaunti ya Serikali wala Shirika linginelo, pili Mhusika lazima awe na Akaunti hai ya Benki yoyote kati ya CRDB au NMB. ambapo wananchi walifurahia jambo hilo na Mkuu wa mkoa akawaambia kwamba, tathimini iliyofanyika ilikuwa ya Shilingi Bilioni 1.5, lakini Fehda iliyokubalika kulipwa na UNHCR ni takribani ya Shilingi Milion 600 , sawa na nusu ya tathimini ya fedha iliyothaminiwa awali. Pamoja na hayo, UNHCR haitakuwa imelipa Fidia bali Kifuta Jasho kwa wahanga.
Nita weka utaratibu mzuri wa kuthibitisha kila mtu na akaunti yake ili kuepuka utapeli wa kufungua akaunti ya mtu asiyehusika, zoezi hilo litakuwa na kutengeneza jedwali litakalo onesha Jila la mhusika, picha, akaunti namba, na sahihi yake, ambavyo vitakuwa vimehakikiwa kwamba huyu ndiye mhusika wa akaunti na ni Mhanga wa tukio alisema Mkuu wa Mkoa"
Malipo hayo yatakuwa tayali mara baada ya zoezi hilo la akaunti kufunguliwa kwa usimamizi mzuri. kama hakuna akaunti malipo hayatafanikiwa alisema Mkuu wa Mkoa, Kisha aliruhusu maswali kwa Wananchi hao na akayajibu yote, Wananchi wakaridhia, kisha kikao kikafungwa.
KIBONDO DISTRICT COUNCIL, KIBONDO TOWNSHIP IHULILO STREET
Anuani ya Posta: P.O.BOX 43, KIBONDO
Simu ya Mezani: +255 028 282 0084
Simu: +255 028 282 0084
Barua pepe: ded@kibondodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Kibondodc .Haki zote zimehifadhiwa.