Ndg: Terry Raphael, Mratibu wa Mazingira Shirika la TCRS Wakimbizi Wilayani Kibondo, amesoma taarifa ya Mradi wa Maji, Afya, Usafi wa Jamii na Mazingira wilayani Kibondo Mbele ya Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya, aliyealikwa kuhudhuria Uzinduzi wa Usafi na Mazingira Wilayani Kibondo iliyozinduliwa rasmi leo tar. 09.11.2017.
UTANGULIZI:
TCRS, iliingia Mkoani Kigoma mnamo mwaka 1981 kusimamia urejeshwaji wa wakimbizi nchini Burundi, lakini ikawa pia inafanya shughuli za maendeleo Kigoma vijijini na baadhi ya Vijiji vya Kasulu. Uongozi wa Mkoa uliomba TCRS ifungue Ofisi Wilayani kibondo kwa ajili ya Maendeleo ya wanchi. TCRS, ilifungua Ofisi yake Kibondo kuanzia mwaka 1986 na kushirikiana na Uongozi wa Wilaya na Wananchi wa Kibondo kwa shughuli za maendeleo, kazi ambayo inaendelea mpaka sasa.
TCRS, kwa ufadhiri wa Norwegian Church Aid (NCA) kuanzia mwaka 2015 ilianza kushirikiana na Idara za Halmashauri ya Kibondo pamoja na Wanchi katika kufanya kazi za WASH (water, sanitation and hygiene) katika vijiji 7 vya Wilaya ya Kibondo na 5 Wilaya ya Kakonko.
TCRS katika Wilaya Kibondo shirika lipo kwenye Vijiji vya Rusohoko, Kigendeka, Kigogo, Nyange, Minyinya, Kumshwabure na Kumsenga. Lakini mwaka 2016, TCRS iliacha kufanya kazi za Maji, Afya na Usafi wa Mazingira kwenye Vijiji vya kumshwabure na Kumsenga kutokana na upungufu wa fedha kutoka kwa Wafadhili, hivyo kubaki na Vijiji 5 katika Wilaya ya Kibondo.
MAFANIKIO:
Kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Idara ya Maji Afya, Usafi wa Jamii na Mazingira pamoja na wananchi katika vijiji husika shirika limefanikiwa kufanya yafuatayo:
CHANGAMOTO:
KIBONDO DISTRICT COUNCIL, KIBONDO TOWNSHIP IHULILO STREET
Anuani ya Posta: P.O.BOX 43, KIBONDO
Simu ya Mezani: +255 028 282 0084
Simu: +255 028 282 0084
Barua pepe: ded@kibondodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Kibondodc .Haki zote zimehifadhiwa.