Kama wanavyoonekana hapo juu pichani.
Anayekabidhi mifuko 100 ya Saruji ni Mkuu wa Wilaya ya KIbondo Mhe. Bura. Akimkabidhi Diwani wa Kata ya Busunzu Mhe. Razalo P. Ntukamazina, huku Diwani Viti maalum CCM
Mhe. Grace Zacharia na Wananchi wote wa Kata hiyo wakishuhudia.
Miongoni mwa nasaha zilizotolewa na Mhe. Bura, katika hafra hiyo, amewataka Wananchi kutumia Vema Misaada inayotolewa na viongozi wa Kuchaguliwa na wale wa kuteuliwa kulingana na matakwa ya Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imejipambanua kupingania haki za wanyonge.
Katika kuonekana kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo hataki masihara na mtu yeyote anayejaribu kukwamisha jitihada za Serikali hasa hii awamu ya Tano ambayo inaondoa kero za wananchi kwa vitendo Bura ameapa kumshughurikia.
Ameyasema hayo baada ya kuridhika na Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Busunzu, kilichopo Wilaya ya Kibondo, wakati alipoongozana na Maafisa ngazi ya Halmashauri na Wilaya siku ya Alhamisi tarehe 16.11.2017, alipokuwa akikabidhi Saruji na kusikiliza kero za Wananchi Kata ya Busunzu.
KIBONDO DISTRICT COUNCIL, KIBONDO TOWNSHIP IHULILO STREET
Anuani ya Posta: P.O.BOX 43, KIBONDO
Simu ya Mezani: +255 028 282 0084
Simu: +255 028 282 0084
Barua pepe: ded@kibondodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Kibondodc .Haki zote zimehifadhiwa.